Senicoms Green Solutions

Senicoms Green Solutions is an integrated business consulting firm that aims at providing creative link in planning and coordination of necessary and helpful business and service information to meet our customer ends at the convenient projected requirements. The agency also opt to provide for various business consulting activities and research on socio-economic development that cater for different services in the field of strategic business planning and development, project planning and write-ups, marketing strategy for product launch and promotion, events management and training on entrepreneurship, leadership skills and career development to our various clients.

On the other hand, the agency also aims at providing logistical services to our clients on job search and recruitment, real estate, procurement, physical movement and storage of components, parts, raw materials as well as semi-finished and finished goods to different clients. Through our communication and logistical strategy we hope to achieve optimum demand-service level at minimal cost that includes inbound and outbound movement logistics, and coordination of business consulting activities to enhance our clients’ oriented expectations.

Tuesday, May 5, 2020

JIFUNZE JINSI YA KUANDAA ANDIKO LA MRADI WA MAENDELEO YA KIJAMII


MAMBO YA KUZINGATIA KATIKA MUUNDO WA ANDIKO LA MRADI NA TAARIFA ZA MSINGI KUHUSU ANDIKO LA MRADI
Je, unaweza kuandika kwa ufupi mambo ya msingi yahusuyo mradi wako? ambayo yanaweza kusomeka kwa wepesi na haraka? yanayoweza kueleweka baina ya mratibu wa mradi na wafadhili au wanufaikaji wa mradi?

(Je, mambo hayo ni yapi? ungana nami katika mtiririko wa somo mwepesi kabisa hapa chini)

(i) Je, unajina la mradi? ambalo ni fupi na jepesi kukubalika la ubunifu na kipekee linalobeba maudhui ya mradi husika.
(ii) Je, una anwani ya taasisi, asasi, kikundi chako?
(iii) Je, una jina na anwani ya mtu anayefanya mawasiliano?
(iv) Je, ni mahali gani ambapo mradi utakatekelezwa? (Mkoa, Wilaya, Kata, Kijiji/Mtaa)
(v) Je, unaeneo la kipaumbele la linaloombewa ruzuku? (kulingana sekta husika zilizoainishwa na mfadhili wako)
(vi) Je, mradi wako upo katika aina gani ya kundi la ruzuku? (kutokana na bajeti ruzuku inaweza kuwa ndogo, kati au kubwa)
(vii) Je, mradi wako unahitaji aina gani ya uwezeshwaji? (kulingana na mahitaji ya muombaji wa ruzuku inaweza kuwa fedha, stadi au vifaa)

(viii) Je, umeandaa muhtasari na usuli wa mradi wako?
(ix) Je, mradi wako unaweza kuwa mantiki na uthibitisho wake?
(x) Je, mradi wako unamalengo gani kulingana na viashiria vya utendaji?
(xi) Je, mradi wako unamatokeo yapi yanayotarajiwa kutoka kwenye utekelezaji?
(xii) Je, mradi wako umewalenga wadau gani ambao wanaweza kunufaika na matokeo ya mradi?
(xiii) Je, mradi wako unampango kazi unao onyesha mtiririko wa shughuli za mradi kulingana na mstari wakati?
(xiv) Je, unampango gani wa usimamizi wa shughuli za mradi wako? unaoweza kuonyesha watendaji wakuu wa mradi pamoja na sifa na ueledi wao?
(xv) Je, mradi wako unampango gani unaohusisha uchambuzi wa mambo mtambuka na wadau muhimu ambao watashiriki katika kufanikisha mradi husika?

(xvi) Je, mradi wako unaviashiria gani vya utendaji wa mradi?
(xvii) Je, mradi wako unavichocheo vipi na vihatarishi vya mafanikio ya mradi?
(xviii) Je, mradi wako unampango gani wa uperembaji na tathmini ya mradi? utakao onyesha bao la mantiki linaloweza kuleta ushawishi wa kukubalika kwa mradi na kufanya wepesi wa ufuatiliaji wa shunguli za mradi?
(xix) Je, mradi wako unampango endelevu unaoweza kuonyesha uendelezaji wa shughuli za mradi hata baada ya ufadhili kuisha?
(xx) Je, endapo mradi wako utafanikiwa kutekelezwa utakuwa na manufaa gani kwa taifa?

UKIFANIKIWA kujibu maswali yote hayo, basi utakuwa umefanikiwa kuandaa andiko la mradi wako na kubakiwa na sehemu kuu moja ya BAJETI ya mradi husika. Ambayo itapaswa iandaliwe kwa mchanganuo mzuri unaosomeka kirahisi (ifafanuliwe kwa kila kipengele), iwe inauhalisia na inayokubalika, inayojielezea kila kipengele kikamilifu, inayoeleweka kirahisi, iwe na uhusiano na mpango kazi (ratiba ya utekelezaji wa mradi), iwe na hesabu za usahihi, na pia izingatie ukweli na iwe inaweza kutetewa.

Kumbuka kuwa taarifa zote hizo zimeandikwa kwa ufupi tu.

KARIBU UJIFUNZE NAMNA YA KUANDAA ANDIKO LA MRADI
(AU TUKUANDIKIE PROJECT PROPOSAL)
EMAIL: senicoms@gmail.com
SIMU: 0787220120

  • Thanks
 Reacti