Senicoms Green Solutions

Senicoms Green Solutions is an integrated business consulting firm that aims at providing creative link in planning and coordination of necessary and helpful business and service information to meet our customer ends at the convenient projected requirements. The agency also opt to provide for various business consulting activities and research on socio-economic development that cater for different services in the field of strategic business planning and development, project planning and write-ups, marketing strategy for product launch and promotion, events management and training on entrepreneurship, leadership skills and career development to our various clients.

On the other hand, the agency also aims at providing logistical services to our clients on job search and recruitment, real estate, procurement, physical movement and storage of components, parts, raw materials as well as semi-finished and finished goods to different clients. Through our communication and logistical strategy we hope to achieve optimum demand-service level at minimal cost that includes inbound and outbound movement logistics, and coordination of business consulting activities to enhance our clients’ oriented expectations.

Tuesday, May 16, 2017

HATUA ZA UPIMAJI WA KIWANJA AU SHAMBA NA KUPATA HATI MILIKI




Ufuatao ni mtiririko wa hatua mbalimbali zitakazo muwezesha mtu yeyote kufanya upimaji wa eneo lake na kupata hati miliki ya ardhi, kwa maana ya upimaji wa kiwanja au shamba hapa nchini Tanzania. Pia yafaa ifahamike kuwa kazi ya upimaji inaweza kufanywa na maafisa wa serikali au makampuni yaliyoidhinishwa na yenye vibali vya kufanya upimaji  wa ardhi kutoka sekta binafsi.

1. Kufanya ukaguzi wa eneo husika
Ili kujua eneo hilo limepangwa kwa ajili ya matumizi gani, atatakiwa atashirikishwa Mpima Ardhi (Land Surveyor) kwa ajili ya kufanya utambuzi wa eneo husika na kujua kama lipo kwa ajili ya matumizi gani. Hivyo ni lazima surveyor afike site/eneo husika na kifaa cha kupimia (Handheld GPS). Atachukua vipimo vya mipaka inayozunguka eneo husika. Baada ya hapo, surveyor ataenda kutafuta taarifa za eneo husika katika ofisi za Halmashauri au Wizarani ili aweze kupata ramani ya mipango miji na matumizi ya ardhi.

2. Matokeo ya zoezi la ukaguzi wa eneo
Eneo husika kukosa sifa za kupimika, eneo husika linaweza likakosa sifa za kupimika kwa kutokua limeandaliwa matumizi kabisa (halina mchoro wa mipango miji), kwa sabababu eneo husika linaweza kuwa lipo katika matumizi ya kijamii mf. makaburi, barabara, soko n.k.

Eneo husika kuwa na sifa ya kupimika, eneo husika kuwa katika matumizi ambayo mtu binafsi anaweza kumiliki mf. makazi, hotel, biashara n.k.

3. Uandaaji wa mchoro wa viwanja, hapa wataalam wa Mipango Miji (Town Planners) watandaa mchoro wa viwanja (Town Planning Drawing) ukionyesha mpangilio wa viwanja vyenye ujazo wa juu, kati na chini (High, Medium and Low Density Plots) ikiwa ni pamoja na miundombinu ya usafirishaji, maeneo ya wazi na soko au biashara. Baadae litaandaliwa file kwa ajili ya kwenda Wizarani likiambatanishwa na ramani ya mchoro wa mipango miji kwa ajili ya kuidhinishwa rasmi kwa upimaji wa eneo husika.

4. Kibali cha upimaji, mteja au mmiliki halali wa eneo husika itabidi aandae barua kwa ajili ya kuomba kupimiwa eneo lake. Barua hiyo itapitia serikali ya mtaa na Halmashauri husika, Iikieleza nia na madhumuni ya kutaka kufanya upimaji wa eneo/shamba lake. 

5. Upimaji wa ardhi, hapa mtaalam wa upimaji ardhi (surveyor) ataweka mipaka katika eneo husika kwa kutumia nondo (pin) au mawe (beacons), pia litaandaliwa file kwa ajili ya kwenda Wizarani likiambatanishwa na ramani ya upimaji na taarifa za muhusika/mmiliki wa eneo. Na mwishowe itarudishwa ramani iliyo hakikiwa toka Wizarani kama ramani ya upimaji wa eneo husika. 

6. Mteja atakabidhiwa ramani ya upimaji, ambayo atapaswa aende nayo kwenye Halmashauri husika na kumuona Afisa Ardhi ili aweze kuandaa hati miliki ya ardhi au viwanja viliyopimwa.

7. Mteja atakabidhiwa barua au hati ya umiliki ardhi, baada ya kupata ramani ya kiwanja na kulipia ada zote za upimaji na umiliki wa eneo husika, mmiliki atapatiwa barua ya umiliki (Letter of Offer) wa kiwanja na hivyo atatakiwa kushirikiana na Afisa Ardhi wa Halmashauri husika ili aweze kuandaliwa jarada la Hati Miliki (Title Deed) ya eneo lake.